![Tusilaumiane](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/08/09/50ee73686d24473e876214a0c1bb9076_464_464.jpg)
Tusilaumiane Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Tusilaumiane - Bright (TZ)
...
Oooh ooooh yeeeh
Mmh
(Verse 1)
Hivi kweli nanipenda? Kwa nini unanidharau?
Kama kweli unanipenda, kwa nini niwe nyang'au?
Nayaona mengi kwenye simu yako ila tu nauchuna
Vimeseji meseji vya mademu wako, jua mi inaniuma
Naskia Mwajuma ana mimba yako, mbona unanitafuna
Lini utaacha hayo mambo yako, mwanaume gani we haya huna, ah
Kama Mimi mtu wa ndani tu, Mimi na ndani tu mbona haya nayaonaa
Kwanini inakutoka Imani boo, hukumbuki nyumbani boo, hivi kweli tutapona
Ukitoka nitoke na Mimi, tusilaumiane
Unayofanya nifanye na mimi eeh, tusigombane
Ukitoka nitoke na Mimi, tusilaumiane
Unayofanya nifanye na mimi eeh, tusigombane
(Verse 2-Bright)
Usione Kobe kainama, kainama nafunga mdomo nisiongee
Sitaki ugomvi kupigana, kuzozana nataka mbele tusonge
Unapenda upinzani Kama Simba yanga, yanga
Ndani hatuelewani tushikiane mapanga, mapanga
Hivi kweli kitu gani Mpaka we unanichamba, nichamba
Eti anapiga Nani mbona hujasevu namba, namba aaah
Nimechoka mapenzi ya Vita kwa nini una visa, haya
Kisirani we kila kukicha mabomu ya Hitler
Mbona yako ninayaona siongei, unajificha unajua sielewi sasa upi upendo wako mama
Mbona yako ninayaona siongei, unajificha unajua sielewi, Unanichiti mume wako, mama
Ukitoka nitoke na Mimi, tusilaumiane
Unayofanya nifanye na mimi eeh, tusigombane
Ukitoka nitoke na Mimi, tusilaumiane
Unayofanya nifanye na mimi eeh, tusigombane
Oooh ooooh tusilaumiane
Tusilaumiane, eeh
added by Renato