Alikuta Ibada Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Alikuta Ibada - Ambwene Mwasongwe
...
Alikuta ibada zinaendelea
Ila zina tatizo
Alikuta maombi yanafanyika
Ila yana kasoro
Alikuta mifungo inaendelea
Ila ina dosari
Akakuta sadaka zinatolewa
Ila zina makandokando mengi
Akashangaa mwili umetawala
Badala ya Roho!
Akawafundisha ibada za Rohoni
Jinsi zitakiwavyo
Muombapo msiombe sala ndefu
Ili watu wawasifu
Mtoapo msitoe kwa matangazo
Ili watu wawaone
Mfungapo msijionyeshe
Ili watu wawasifu
Ila baba yenu aliye sirini
Yeye atawajazi
Mungu ni roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu
Kwa roho na kweli
Yeye huona kile ambacho jicho haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
(Kwake hakuna siri)
#
Akawakemea Viongozi wa dini
Na washika sheria
Waandishi na mafarisayo
Na masadukayo
Hawakutaka-Walikasirika
Wakaleta vitabu
Kwa mamlaka ya nani wafanya haya?
Wapate kumshitaki
Wakadhani kiroho ni shule
Ili wamfedheheshe
Akawatazama akawapima
Walikuwa weupe
Wakamletea mwanamke mzinzi
Aliyefumaniwa
Wakataka wasikie neno lake
Atakavyomuhukumu
Akainama akachora chini
Akaandika majina yao
Ardhi ikageuka "video touch"
Wote wakakimbia
Mzee wa kanisa alipojiona
Akilewa na wake za watu
Shemasi kaona aibavyo sadaka
Naye akakimbia
Wanakwaya wakaona wanavyosengenyana
Na kupiga majungu
Yesu alipoinuka
Wote wamekimbia
Akasema na mimi sikuhukumu
Nenda usitende dhambi tena!
Ole mafarisayo na masadukayo
Mwaosha vikombe kwa nje
Ila ndani ni vichafu
Mwapaka makaburi chokaa
Ndani yake ni mifupa
Mwawabebesha watu mizigo
Ninui hambebi
Ole!
Mwawatungia wengine sheria ninyi hamzifuati!
Ey!
#
Akalikaribia kapu la sadaka
Aone wanachotoa
Ghafla akamwona mwanamke mjane
Anatoa kichache
Akasema huyu ametoa vingi
Kuliko ninyi nyote
Maana kwa Mungu wingi sio idadi
Ni ukamilifu wa jambo
Wengi mmetoa kwa mbwembwe
Vimeonekana vingi
Ila mlivyobakisha nyumbani ni vingi
Sio kama mwanamke huyu
Akaona wanagawana chenji ibadani
Akakasirika
Wanauza vitu kama mnada hekaluni
Mahali pa ibada
Akachukua fimbo akawachapa
Akapinduapindua
Nyumba yangu itakuwa ya sala
Sio nyumba ya biashara
Uko wapi moyo wa ibada?
Uko wapi moyo wa kicho!?
Ule moyo wa kutetemeka
Tusikiapo neno la Bwana
Mambo haya Je yamo kanisani leo basi tujiulize
Akija yule mwenye kanisa
Je hatatuchapa?
Mungu ni Roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu kwa roho na kweli
Maana yeye huona kile ambacho jicho
Haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono
Hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
#
Tunatakiwa tumwabudu Bwana
Tusichonge sanamu
Tuangalie tusije kujiabudu wenyewe
Pamoja na vitu vyetu
Tukicheza ili watu watuone
Tumejiabudu wenyewe
Tukiimba ili watu watufurahie
Tumetwaa utukufu
Tukigeuka nyuma na kutafuta maoni ya watu
Tumejichuuza wenyewe
Hicho ndicho kilichomponza lusifa
Alitaka asifiwe
ooh!
*