![Mfalme Wa Amani](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/3D/26/rBEeMllLddqAYGFAAACYKNUQWgA284.jpg)
Mfalme Wa Amani Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2017
Lyrics
Mfalme Wa Amani - Solomon Mkubwa
...
Daudi kasema nilikuwa kijana sasa ni mzee
Daudi kasema nilikuwa kijana sasa ni mzee
Sijawahi ona mwenye haki ameachwa mimi
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani
Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake wanadamu
Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake si kama wanadamu
Akiongea Yesu ameongea
Akikuahidia kitu Baba ameahidi na ujasiri aah
Atatenda kwa wakati wake yoyoo
Ninamwita Bwana wa amani yeyeyee
Ninamwita mfalme wa amani Bwanaaa
Ndio maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake
Ni uwezo gani,uwezo gani unaompinga Yesu
Uwezo gani,uwezo gani,uwezo gani
(Chorus)
Mfalme wa amani mfalme wa amani uinuliwe
Wewe ni mwema ,wewe ni mwema Bwana wangu*4
Usilie, usilie, usilie wewe
Usilie Bwana anakujua ndugu yangu
Amesikia kilio chako wewe mama
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu
Wanadamu hawatakusaidia na kitu
Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote wewe
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake
Ni yule mfalme wa amani
Ni yule aliyesema yote imekwisha
Mambo unayoyapitia ni yeye anayeyaona
Anajua shida yako mama yangu
Anajua magumu yako baba yangu
Ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia
Ukiwa na magumu usiende kwa wafumu wa dunia
Muite mfalme wa amani yeye, anajibu maombi
Muite mfalme wa amani yeye, anajibu maombi
Ni uwezo gani ,uwezo gani unaompinga Baba
Uwezo gani ,uwezo gani ,uwezo gani
(Chorus)
Mfalme wa amani ,uinuliwe Bwana wangu
Yale unayotenda yashangaza dunia nzima
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao uwape amani
Wanaokosa amani ndani ya kazi zao uwape amani
Ni wewe Bwana wa amani ya kudumu
Ni wewe Bwana wa amani ya Afrika
Amerika wanalia amani
Tunawe Bwana mfalme wa amani
Tunawe Bwana mfalme wa amani
Hakuna kitu kile kinachokushinda Bwana
Yeye Mfalme wa amani
(Chorus)