![Mapito](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/05/12/11d5cd74b20345b8a8e31a135b16a5c9.jpg)
Mapito Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2017
Lyrics
Mapito - Christina Shusho
...
Ni mapito
Mapito ya dunia hii
Ni mapito unapitishwa tu
Unayoyaona
Ujue ni mapito ndugu
Mapito yako
Kipimo cha imani
Ni mapito
Mapito ya dunia hii
Ni mapito unapitishwa tu
Unayoyaona
Ujue ni mapito ndugu
Mapito yako
Kipimo cha imani
Futa machozi
Ujue ni mapito ndugu
Unayelia kumbuka hayo ni mapito tu
Mapito yako
Kipimo cha imani yako, ooh
Jipe moyo Mungu yuko nawe
Mungu wetu si kiziwi hata asisikie
Anajua unayoyapitia
Jipe moyo yeye yu pamoja nawe
Ushindi wako umekaribia
Ni mapito
Mapito ya dunia hii
Ni mapito
Unapitishwa tu(Jipe moyo ndugu yangu)
Unayoyaona
Ujue ni mapito ndugu(Ni jambo moja tu)
Mapito yako
Ni kipimo cha imani
Ni mapito
Mapito ya dunia hii (Kweli tunapita)
Ni mapito unapitishwa tu
Unayoyaona (wewe)
Ujue ni mapito ndugu
Mapito yako
Kipimo cha imani
*****
Haijalishi leo hii unapitia nini,
Wengine kati yetu wanapanda mlima ,wengine wanashuka
Lakini katika yote unayoyapitia maishani mwako Jipe moyo simama kwa imani,
Mtumaini Bwana maana mapito unayopita leo ni kipimo cha imani
****
Jaribu halikuwapata isivyokuwa kawaida ya mwanadamu
Lakini Bwana hutuondoa nayo yote
Nasema nawe
Jipe moyo
Songa mbele
Futa machozi
Ushindi wako umekaribia
Hata kama jaribu lako limekuwa kubwa kama mlima
Yeye Yesu atafanya mlango wa kutokea
Adui ajapo kwa njia moja atatawanyika kwa njia saba
Jipe moyo Mungu yupo nawe
Ni mapito
Mapito ya dunia hii
Ni mapito unapitishwa tu
Unayoyaona
Ujue ni mapito ndugu
Mapito yako
Kipimo cha imani
Ni mapito
Mapito ya dunia hii
Ni mapito unapitishwa tu
Unayoyaona
Ujue ni mapito ndugu
Mapito yako
Kipimo cha imani
¶¶¶¶¶¶