![Bado](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/03/15/eaf5450e492742298354b8fa4ebf2297.jpg)
Bado Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Bado - Rose Muhando
...
lyric sync by Phellow 254790511905
Nini ?
je, mnataka kuona nini?
nauliza mnataka kuona nini?
wasomi mwatakaje kuona nini?
kanisa linataka kuona nini?
ndipo mjue yametimia
dunia eh kama kulemewa, imelemewa sana
dunia eh kama kuanguka, imeanguka sana
hivi mnataka kuona nini?
ndipo mjue yametimia
dunia inataka kuona nini
ndipo mjue Mungu anasema
mbona akili za wenye akili
zimefika kikomo jamani
maarifa ya wenye akili yameshindwa kabisa
hekima ya wenye hekima haisaidii kitu
hivi mnataka kuona nini
nauliza mnataka muone nini
ndipo mjue Mungu anasema
bado
kama ni mapigo
bado
kama ni magonjwa
bado
kama timbwilitimbwili
bado
kama ni hekaheka
bado
msishangazwe na ya leo
bado
baragumu ya kwanza imekwisha kupigwa
dunia ijipange
baragumu ya kwanza imekwisha kulia
kanisa lijipange
na hapa ndipo penye imani
na subira ya watakatifu wajipange
mwenye masikio na asikie neno hili
roho asema mjipange
bado
ni ishara tu
bado-ooo
basi inueni macho yenu
tazama vilele vimeinama
wafalme wamechanganyikiwa
wenye akili hawana la kufanya
manabii maono yamekoma
ufunuo maono yamekoma-aaa bado
haya sasa dunia yote mikono juu
semeni Mungu pekee ndiye Bwana
basi inueni macho yenu
tazama vilele vimeinama
wafalme wamechanganyikiwa
wenye akili hawana la kufanya
manabii maono yamekoma-aaaa
ufunuo maono yamekoma-aaa bado
*******
nani basi asimame
mbele za Mungu aseme
alete hoja nyingine
ashindane na Mungu tuone
maneno ya Mungu kamwe hayatapita
nasema mjipange
kengele ya hatari imekwisha kulia
jamani mjipange
bado
ni ishara tu-uuuu
bado
na magonjwa bado
bado
na shida bado
bado
njaa na matetemeko
bado
msishangazwe na ya leo
bado
msishitushwe na ya leo
bado
ah na anasema bado
bado
wuuuuwiii
bado
hoyeeee
bado
yeeeee
bado
lyric sync by Phellow 254790511905