![Mawazo ft. AY](https://source.boomplaymusic.com/group1/M04/AB/71/rBEehlzBfvCAER0EAADgRuzrqcE18.jpeg)
Mawazo ft. AY Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2003
Lyrics
Mawazo ft. AY - Lady Jaydee
...
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
mawazo ooh mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
swala ambalo liko palepale ni mawazo
Hata ukiwa na pesa lazima uwaze utapanga bajeti ni nini ukafanye
ukiwa hunazo pesa ndiyo Yazidi utawaza ni wapi uende ukasake
Toto lako likiwa tukutu utawaza ulichape viboko vingapi ili likome
walimwengu nao wakiwa wakusakama utawaza ni jinsi gani uwaepuke
hakuna binadamu asiye na mawazo hata vichaa nao pia huwa wanawaza
kila kitu Duniani lazima uwaze
hakuna litendekalo bila ya mawazo
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
mawazo ooh mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
swala ambalo liko palepale ni mawazo
tukitembea na tukikaa tuna mawazo
Hata mimi ladyjaydee nina mawazo (sex lady jide uuh)
wazo langu nataka nunua freelander ila si lazima wazo langu litimie
wengine wawaza kuiba watajirike
wengine kuwa warembo wasifike
Amita anataka kuwa
Amina kuwa mtangazaji maarufu
Toyoyo kujenga nyumba ya kifahari
Renee hata yeye kuishi na mzungu
kila mtu Duniani lazima uwaze hakuna litendekalo bila ya mawazo
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
mawazo ooh mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
swala ambalo liko palepale ni mawazo
tukitembea na tukikaa tuna mawazo
mawazo ooh mawazo
mawazo na mi, mi na mawazo
Hayo ndio maisha yangu kila siku wa commercial
Inanitinga mpaka naonekana ka mjinga
always deal zinakataa lakini haiko mkinga
nikitembea nikiongea kichwa changu chawaza
Yani mawazo kibao yani hadi ya kuwaza
nawaza kuhusu maisha
wapi ntapata pesa wapi zilipo sasa na ni vipi ntazinasa
mara nyingine mi nadata maisha yanielemea wengine wananicheka
oh oh oooh
tushasikia wengine washajitoa roho
machoni naona giza unafuu hata siuoni
msaada nitapata wapi kwenye shida hatujuani
Wengine wanaongea peke yao njiani yote kuwaza, yote kuwaza tu
Mawazo kila mtu anayo mawazo (uuh jaydee na mawazo)
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
mawazo ooh mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
swala ambalo liko palepale ni mawazo
tukitembea na tukikaa tuna mawazo
mawazo ooh mawazo