![Siku Hazigandi](https://source.boomplaymusic.com/group2/M04/BF/8A/rBEeM1zBeGiAKs_ZAACN69RhGi8984.jpg)
Siku Hazigandi Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2001
Lyrics
Siku Hazigandi - Lady Jaydee
...
Yote mliyosema yote mliyotenda aah
nasahau
mangapi iii yamesemwa mangapi nimeona
mmh..mliyosema aah nasahau kwani siku uh hazigandi yamesemwa mangapi
maneno na vyenu vicheko vitapita kama upepo
Yote mlotenda wapendwa kusahau nimeamua
kujitenga na yasonifaa kuanza maisha mapya
Hayo mliyokwishayajua ishieni hapohapo
Kila mtu ana dhambi hakuna aliye haki
Kusemwasemwa sitaki mnanipotezea bahati
Yote mliyosema yote mliotenda aah nasahau
mangapi iii yamesemwa mangapi nimeona
mmh..mliyosema aah nasahau kwani siku uh hazigandi yamesemwa mangapi
Sitowapa tena nafasi kunijua sana undani
wala sitalipa kisasi Mola anajua kwanini
na tena sirudi nyuma ili kuyakwepa ubaya
kwangu moyo unanituma yote hayo kuyaacha nyuma
Ooh siku hazigandi hakuna aliye haki, kila mtu ana dhambi hakuna aliye msafi.
Yote mliyosema yote mliotenda aah nasahau
mangapi iii yamesemwa mangapi nimeona
mmh..mliyosema aah nasahau kwani siku uh hazigandi yamesemwa mangapi
Yamesemwa mangapi
Yamesemwa mangapi
Yamesemwa mangapi
yamesemwa mangapi