![Usikatae ft. Dully Sykes, Mr. Blue, Mad Ice & Dorice](https://source.boomplaymusic.com/group2/M04/BF/8A/rBEeM1zBeGiAKs_ZAACN69RhGi8984.jpg)
Usikatae ft. Dully Sykes, Mr. Blue, Mad Ice & Dorice Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2001
Lyrics
Usikatae ft. Dully Sykes, Mr. Blue, Mad Ice & Dorice - Lady Jaydee
...
Maisha kwa wengineo huwa matamu
Lakini kwa wengine huwa magumu
Jiulize ndani ya moyo ni kwanini
Maisha yawe ya utofauti
Fungua macho mpe mkono
Fungua moyo toa kidogo
Chochote kile ulicho nacho
Si utajiri bali ni moyo
Aiyo iyo iyo iyo mama iyo
Dunia hii wote tunapita
Nani wa kusema anajivuna
Asiyekufa chini akazikwa?
Labda kesho zamu yako
Mpe leo akupe kesho
Ikifika kesho asipokuwepo
Thawabu peponi yakungoja we
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yanakukuta
Dunia yabadilika wewe
Yabadilika
Kama wote tulizaliwa Afrika, oh ooh
Basi sote ndugu wa mama mmoja
Tusaidiane
Tulipinge balaa hili lilotukuta
Tuokoe ndugu zetu watanzania
Mimi leo naanza kwa kuimba mmh mmh
Baraka ishuke kwetu, balaa liondoke kwetu
Furaha ije tena kwetu, mateso mateso sasa basi!
Itika anapokuita, zaidi ya upoweza
Dunia yabadilika, hujui lini utaanguka
x2
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Dunia yabadilika
Usikatae akikuita
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka