![Ndoa ft Khadija Kopa,Juma Karere,Karen](https://source.boomplaymusic.com/group1/M15/7A/7C/rBEehl43wUSAetplAADbi7peups467.jpg)
Ndoa ft Khadija Kopa,Juma Karere,Karen Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2020
Lyrics
Ndoa ft Khadija Kopa,Juma Karere,Karen - Bright (TZ)
...
Mwanangu vipi baba mbona kimya baba
Uliahidi jambo mbona kimya baba
Mambo ya ndoa umefikia wapi baba
Mambo yako ya ndoa umekwama wapi niambie
Nimezunguka dunia nzima dunia kiganja baba
Nimeyaona mengi
Ya walimwengu wanasema bora uchague mpenzi tofauti na enzi
Wanafanana kwa sura matendo baba niko hoi eee
Unayempenda anakukwaza ye anamuwaza mwingine
Bila pesa umaarufu mwonekano baba we hung'oi ee
Na Kwa dunia ya sasa nioe wapi pengine
Dunia hadaa ilo baba utambue
Muda unaenda hilo uzingatie
Mweke maulana mbele mambo yatimie
Dhamira yako ya kweli nayo ajalie
Baba oo baba oo daddy oo (baba)
Najua una hamu sana (mwana)
Ndoa oo ndoa oo ndoa oo
Yami mwanao kuiona
Kaza roho kaza roho dua njema atajibu maulana
Mke mwema atakuja tu baba
Aeee (aeee) ndoa eee (nuwia baba)
Sijamwona wa kuoa eee (utaoa mwanangu)
Aeee (aeee) ndoa eee (nuwia baba)
Sijamwona wa kuoa eee
Na yote na ??dafaradhi mwana lisha mwanangu
Kwangu mimi ni heshima nikimwona mkwe wangu
Kudangadanga si kwema kwaleteana laana mwanangu
Leo Ali kesho Juma ebu tunza utu wako
Mama wakitongoza wanataka kuvuana nguo
Ati tumejuana leo anataka kunivua nguo ee
Wanaume wa sasa suruali kushuka
Mama niombee kwa mungu nipate mwema aniweze sitirika
Aaah niletee mjukuu nilee aje anikojolee oooo ooooh
Mama oo mama oo mama oo najua una hamu sana
Ndoa oo ndoa oo ndoa oo yami mwanao kuiona
Kaza roho kaza roho dua njema atajibu maulana
Mume mwema atakuja tu mama
Aeee ndoa ee (nuwia mwana)
Sijamwona wa kunioa ee (oooh nuwia mwana)
Aee ndoa eee (sijamwona wa kunioa)
Sijamwona wa kunioa
Asee mama mama mama mama Aeee ndoa ee (sijamwona wa kunioa)
Sijamwona wa kunioa ee
Utampata baba alokuridhia
Nataka nicheze (mwanangu)
Siku hiyo ya miede ee (mwanangu ee)
Nikate nikate kwa furaha yangu eehe