
Hautoniacha Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Nashukuru kwa kuwa umeniumba Baba,
kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha sana,
ulinijua tumboni mwa mama,
ukaniweka, ukasema mwanangu zidi kukua,
Nije nikutumie nipendavyo mie.
Na
Ulisema Hutoniacha,
Wewe ni mwanga kwenye giza waangaza,
Utashuka na Malaika,
shida zangu zote Baba wazijua,
Hata nikianguka naita Bwana,
Uwepo wako ndani yangu wanitosha,
wewe ni nguvu tena ni mwamba,
mimi ni jiwe wala sitotikisika.
Owh ooh
Sababu we ni Bwana aah
Sababu we ni Bwana aah
Bwana aah Bwana
Sababu we ni Bwana aah
Ulisema Hutoniacha,
Wewe ni mwanga kwenye giza waangaza,
Utashuka na Malaika,
shida zangu zote Baba wazijua,
wewe ni nguvu tena ni mwamba,
Uwepo wako Bwana wanitosha.
wewe ni nguvu tena ni mwamba,
Uwepo wako Bwana wanitosha.