![Mazonge ft Jolie](https://source.boomplaymusic.com/group2/M01/0A/80/rBEeqFrZviSABoMPAACeWpuDF34882.jpg)
Mazonge ft Jolie Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2018
Lyrics
Mazonge ft Jolie - Bright (TZ)
...
Wee nipende hivyo hivyo mamaa
Japo mambo ndivyo sivyo mamaa Punguza na masikitiko sanaaa Tupendane mpaka kifo mamaa
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Jana tumelala njaa
Paka amelala jikoni
Kibanda chetu chavujaa
Usiku tunalala kihunii
Ulisema utanipenda mpaka mwisho Hutonikimbiaa yaaah
Na hali yangu ni ngumu mahangaiko Utavumilia yaah
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Mbona nayona mengi natamani Lakini natuliza moyooo
Japo wanasema mengi majirani Napuuza naachana nayooo
Mwenye nacho anaongezewa (eeeh) Urefu wa kamba nasubiria
Bila Imani utanikimbia mpenzi
Kwa hii hali nachechemea
Shilingi yaua mume wangu
Mlinzi nalinda pendo langu
Japo kidogo ndo cha kwangu Mungu anajua kesho yangu
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Nakupenda hivyo hivyo Baba
Japo mambo ndivyo sivyo Baba Hata na mahangaiko hayaaa Ntakupenda mpaka kifo Baba
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Kazi nimefukuzwa
Kibarua kimeota nyasi mamaa
Joto lanifukuta
Mfukoni sina hata hela ya ngama Nasikia mama mwenye nyumba nae Anataka kodi yake Hivi kweli Mazonge yamepitiliza Na sipati jibu lake saa nafeli
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Piga konde baba Kidogo ndo ujaza kibabaa
Ridhiki mafungu saba
Tunachopata tushukuru si haba Ukweli kusema nakupenda tu
Sijali kwa hali iwe chini ama juu Wao kwa magari sisi kwa miguu Tule kachumbali miguu ya kuku (Huuu huuu)
Mkono mtupu haulambwi baby Utanipenda vipi
Penzi tupu bila pesa halitambi Utanielewa vipi
Nimeamini kweli wee kipenda roho Na nyama mbichi imenikaba koo Tule kiporo (aaah eh)
Giza totoro (yaa wee)
Uuuh mama yee ... Mmmmh
Wee chaguo langu
Wee baba wee… Wewe mwandani wangu
Nitakupenda milele...
Unipende milele
Nitakupenda milele...Iyee iyee iyee... Aaaah eeehhh….. Aaaah eeehhh Uuuuhhhhh… uuuhhhhhh….
Uuuhhhh... mmmmh mmh
en/bright-mazonge-lyrics