![Nimewasamehe](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/09/E6/rBEezlrF-cCAKdQ4AADcDCQ5mDk748.jpg)
Nimewasamehe Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2018
Lyrics
Nimewasamehe - Solomon Mkubwa
...
nilipokuwa mtoto, nilizaliwa kama wewe
viungo vyote vya mwili vilikuwa kama wewe,
ghafla ya dunia mamno yakageuka
nikajikuta kiungo kimoja kimeniondokea
mimi nikajua kuwa mwisho wa mambo yote umefika
wala sifai, nikaona dunia imenitupa, nikaona dunia imenidharau nikajidharau mwenyewe
nikajua sasa mimi sifai tena
niliwanung'unikia wote waliohusika
kwa haya mambo roho ya kisasi ikaja juu yangu
nikajua sasa na mimi nitalipa kisasi
kumbe kunae Mungu, Mungu wa visasi
akaniambia Solomon nina mpango na wewe
lazima piga hatua uwasamehe kwanza
ooh nikabishana na Mungu wote walionitendea mabaya
mimi siwezi wasamehe moyoni mwangu
bwana akaniambia wataka nitumike na wewe
nina ahadi nzuri na wewe, kuhusu dunia hii
ukitaka nitumike na wewe, waachilie wote
uliowaweka moyoni mwako, nikapiga hatua
nikawasqmehe wote walionikosea bwana akatumika na mimi ooh, ooh
nimewasamehe wote , nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu
nimewachilia wote, nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
nimewasamehe wote, nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
tumekunywa damu,damu ya yesu tumekula na mwili wa yesu,
mwili wa yesu ni msamaha,tujikane wenyewe
mara nyingi tumeonekana wajinga duniani
dunia imeshindwa kutuelewa wakristo
umetendewa mabaya, lakin neno linasema
kubali nenda kaomba msamaha
kikawaida ya dunia,ukinitendea mabaya
lazima ooh iyeleweke, lakin kwetu sisi wakristo
ukinitendea mabaya mimi lazima nikusamehe
sababu nisipokusamehe, baba yetu wa mbinguni na yeye hawezi nisamehe, haijalishi unapitia nini
kama wewe umeokoka uwasamehe walio kukosea usifanye moyo wako jela
kuwafungia watu amua leo uwaondoe
ili Mungu wetu akubaliki, samehe jiran yako mungu na yeye atakusamehe
nimewasamehe wote, nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon
nimewasamehe wote, nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
nivigumu jaman mara nyingi
kuna mambo ambayo tunayapitia
mwenzako mwanadamu anakupitisha kwa mambo mazito lakin unapaswa ufanyeje
ashukuriwe Mungu sababu neno la Mungu linasema tusamehe tu, na tulivaa mwili wa yesu
tumekunywa damu ya yesu, kumbuka msalaban yesu aliwaponya watu, viwete wakatembea
mabubu wakaongea, akawalisha watu
zaidi ya elfu tano, lakin wale watu ndio walimuweka msalabani, msalabani akasema baba uwasamehe, kumbuka stephano, stephano alikuwa anapigwa mawe, alivyokuwa anapigwa mawe, biblia inasema, staphano akamwambia baba uwasamehe, maana hawajui wanalolitenda
na biblia inasema stephano akaona mbingu zinafunguka kwenye msamaha kuna nguvu
kwenye msamaha kuna uwezo stephano hakujali twna mawe wanayomtupia, wanayomchapa
lakini stephano alikuwa ameona mbingu
zinafunguka na tayari anakwenda kupokelewa
samehe jiran yako, kusudi uone mkono wa Mungu usimfungie kwenye moyo wako
utakuwa umejizuilia baraka yako
msamehe mwachilie tu maan tulivaa mwili wa yesu, na tumekunywa damu ya yesu
ooh yesu tusaidie kuwasamehe waliotukosea
mmh pengine una watu ambao umefungia moyoni na hutaki kuwasamehe
nakwambia leo fungua moyo wako ili Mungu wa mbinguni akusamehe
usijiwekee vikwazo, maisha ni mafupi
yesu yu karibu kuja, uwasamehe wote
waliokukosea ili uone mbingu ooh
hatujui ya kesho yakesho ni ya Mungu
fungua moyo wako leo, yule ulie mkopa ela
kashindwa kurudisha, sasa leo amekutusi eeh
na yeye umsamehe, uwe safi mbele ya Mungu
yesu yu karibu kuja, uwasamehe wote
nimewasamehe wote, nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
nimewasamehe wote nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
nimewasamehe wote nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu
nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu
nimewasamehe wote nimewasamehe wote
nimewasamehe kutoka moyon mwangu nimewachilia wote nimewachilia wote
nimewachilia kutoka moyon mwangu