![Yahwe Uhimidiwe](https://source.boomplaymusic.com/group1/M01/6D/87/rBEeMVqmK5aARCa0AADpBo8ZPAU287.jpg)
Yahwe Uhimidiwe Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2013
Lyrics
Yahwe Uhimidiwe - Angela Chibalonza Muliri
...
Yahweh uhimidiwe
waaminifu wako umejulikana
kwa mataifa yote ya ulimwengu Yahweh×2
Uliumba lakini haukuumbwa
jina lako Jemedari ninakuinua
jina lako mkombozi ninakupenda
umefuta jina langu kwenye hukumu
umefuta jina langu kwenye laana
ndio maana ninakuinua Mungu wangu eeh
kwa sanabu siko tena chini ya dhambi eeh
CHORUS
Kama sio wewe Yesu ningeitwa nani
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi
kama si wewe Yesu ningeenda wapi
kama si wewe Baba ningesema nini
Asante Bwana Yesu kwa ukombozi
Asante Bwana Yesu kwa wokovu
ndio maana nakuinua Mungu wangu eeh
umeniokoa mimi kwa damu ya bei
umenitendea mambo ya ajabu eeh
ninakuinua Baba yangu
CHORUS
Majina yote mazuri ni yako baba eeh
unaitwa Jehovah Shammah ninakupenda
unaitwa Jehovah Jireh ninakupenda
unaitwa Jehovah Nisi bendera ya ushindi wangu
asante baba yangu kwa upendo wako
hakuna mwingine kama wewe × 2
ninakupenda Baba yangu
CHORUS