
NINAKUMBUKA SAYUNI Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
NINAKUMBUKA SAYUNI - Papi Clever & Dorcas
...
1.Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri mbinguni
bahari kama kioo na furahia rohoni
Nyuma kimeta cha nuru Naona mji wa mbingu
nyimbo za nyumba ya Baba nasikiliza daima
(Mapambazuko mbinguni yataondoa utaji
vyote tulivyoamini tutaviona milele)*2
2
Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu
yeye aliwakomboa wote; wafalme, watumwa
Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida
mbavuni mwake nafasi kama bandari salama
(Mapambazuko mbinguni yataondoa utaji
vyote tulivyoamini tutaviona milele)*2
3
Kuna jaribu njiani, mengi yakunizuia
na mara nyingi miiba, inaumiza miguu
(Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa
Mbinguni naitazama na kuhimiza safari)*2
(Mapambazuko mbinguni yataondoa utaji
vyote tulivyoamini tutaviona milele)*2