![Napokea Kwako ft.Christina Shusho](https://source.boomplaymusic.com/group2/M00/66/44/rBEeNFpgS3KACch8AADOFO_rufs961.jpg)
Napokea Kwako ft.Christina Shusho Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2013
Lyrics
Napokea Kwako ft.Christina Shusho - Janet Otieno
...
Maisha magumu sana nimepitia
Nikajaribu kutafuta msaada sikupata
Nikaendea mwanadamu mwisho wake ni dharau
Kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu
Nilijua wako wenye haki ya kubarikiwa tu
Kumbe baraka ni haki ya kila mmoja
Nimebadili wazo langu namuelekea Mungu
Kwake msaada wangu unapatikana
Msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi
Nami zamu yangu kubarikiwa weee
Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Yesu napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Nimeamua kwenda zaidi na zaidi
Nimejipanga hadi nione matunda yake
Yale Mungu amewekeza ndani yangu
Najua Mungu yuko kazini kunikamilisha
Akisema nimebarikiwa nimebarikiwa tu
Hata ukipinga wewe leo mimi nimebarikiwa tu
Mlima gani kuu sana usioung'oa (usioung'oa eee)
Jaribu gani gumu sana usiloliweza (usiloweza Mungu eee)
Chozi gani zito kwako usilolifuta (chozi zito lipi hilo)
Ombi gani kubwa sana usilolijibu
Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako
Baraka yangu Baba napokea kwako
Napokea kwako
Ada yangu Baba napokea kwako
Napokea kwako
Utajiri wangu Yesu napokea kwako
Napokea kwako
Elimu yangu Baba napokea kwako
Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Kazi yangu Baba napokea kwako
Napokea kwako
Na watoto wangu Yesu napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Yesu napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Baba napokea kwako
Napokea kwako
Yesu napokea kwako