Diamond platnumz (Zuwena) Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2023
Lyrics
Diamond platnumz (Zuwena) - pittyBoy
...
habari gani kaka
naamini unaniskia
mi mzima wa afya
mama Mungu anasaidia
toka ulipotuacha mahututi anazidiwa
Bibi presha presha nae alatangulia
bado twakuombea ulale salama pema
japo moyoni nina dukuduku natamani kusema niseme eeh
zile mali ulizousia ulizotuusia tuligawa salama
Zuwena zote tukampatia tusiwe ndugu lawama ila Zuwena kaka amebadilika Sana yani shem lake bi zuu wa Leo sio yule wa Jana
chorus:
natamani ungemwona(Zuwena)
japo ungemwona (Zuwena)
kidogo tu ungemwona(Zuwena)
ungemwona (Zuwena)
oooh ungemwona(Zuwena)
zuwena (Zuwena)
oooh ungemwona (Zuwena)
zuwena (Zuwena)
Zuwena sasa kawa chotara
sio tena cheusi mangara
ngozi kaichupua awe mzingu anavuta na sigara
mara boko mwananyamala
anachezesha tu miamala
kutwa anaisugua kipepe rungu tena peku bila ndala
Zuwena skuizi anabandika kope(Zuwena)
Zuwena mipasuo Kama yote(Zuwena)
Ooh Zuwena lipa shika tuondoke(Zuwena)
Aaah Zuwena wanamtaja wote ooh
Juzi kabebwa kwa majirani hata hajitambui(Zuwena)
Yani kalewa tafarani??????(Zuwena)
Zuwena tena sio wa ibada na dini
sadaka chenji aisaidie
sikuizi kageuka pedeshe wa mjini
kutunza bendi wamsifie
na like gari lako urithi wa Babu
la kulishia ng'ombe
skuizi Kama kwato kwenye vilabu linabebea pombe
mama tete kitandani hata hawezi kutembea
Zuwena ameshindwa kuja kumwona Panadol kumletea
chorus
skuizi kataradadi(anadanga anakula ndizi kwa maganda)
anajiita JLo(anadanga anakula ndizi kwa maganda)
Eti mzungu mweusi(anadanga anakula ndizi kwa maganda)
anatunyosha baba(anadanga anakula ndizi kwa maganda)