![KESHO ft. Guardian Angel](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/01/23/899f0267a5b046008225c6fcd8e27b86H3000W3000_464_464.jpg)
KESHO ft. Guardian Angel Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Kesho ni ya Mungu
Ipo mikononi mwake
Kesho ni ya Mungu
Wewe usijali usijali eh
Mungu yuko na wewe
Usijali usijali eh
Mungu yuko na wewe
Itakubidi uyasahau ya jana
Yalishapita basi tugange yajayo
Ukiomba we amini usitie wasiwasi
Ukimuomba kwa siri atakujibu kwa wazi
Shukuru usilalamike alishanena nani apinge
Shukuru usilalamike eeei je je je
Walikosea walipokucheka ila wao hawakutambua aaah
Kesho ni ya Mungu
Ipo mikononi mwake
Kesho ni ya Mungu
Wewe usijali usijali eh
Mungu yuko na wewe
Usijali usijali eh
Mungu yuko na wewe
Motivational speakers wananiambia nisave
Jinyime leo utakula kesho
Ila birds of the air hawananga pa kusave
Kesho ikifika bado wanapiga sherehe
Ina maana we uko safe tangu mungu akusave
Pesa yako ndani ya safe ukiamka una set combination yeah
Mungu ameshakusetia meza usijali
Kesho ni ya Mungu
Ipo mikononi mwake
Kesho ni ya Mungu
Wewe usijali usijali
Mungu yuko na wewe
Usijali usijali
Mungu yuko na wewe
Wewe usijali usijali eeh
Mungu yuko na wewe
Usijali usijali
Mungu yuko na wewe