![Nimepata Bahati](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/4C/4D/rBEeMVnKPICARD0WAADGEz_rTzs793.jpg)
Nimepata Bahati Lyrics
- Genre:Taarab
- Year of Release:2014
Lyrics
Nimepata Bahati - Johayna Abdallah
...
.....
nimeipata bahati aaaaallah aaa
mola amenishushia aaa aaallah
moyo ametia nuru aaaaaallah aaa
imani imeingia aaa aaallah
nilikuwa nimeaswi,maovu nikaingia
sikuwa na wasiwasi,nilitazama dunia
nilikuwa nimeaswi,maovu nikaingia
sikuwa na wasiwasi,nilitazama dunia
ewe mpokea toba aaaallah aaa
ewe bwana wa mabwana aaa aaallah
kwako ninafanya toba aaaaallah aaa
nimekuja maulana aaa aaallah
nilihadaa dunia,nikasahau na mungu
leo ninaangukia,nisamehe dhambi zangu
nilihadaa dunia,nikasahau na mungu
leo ninaangukia,nisamehe dhambi zangu
wewe ni msamehevu aaaaallah aaa
dhambi utanifutia aaa aaaaallah
mola nipe utulivu aaaaallah aaa
kaburini nikiingia aaa aaaaallah
unipe kauli njema,katika mdomo wangu
unifanye mja mwema,nakuomba mola wangu
unipe kauli njema,katika mdomo wangu
unifanye mja mwema,nakuomba mola wangu
dumisha ibada kwangu aaaaallah aaa
niwe mwenye kutubia aaa aaallah
unifanye mchamungu aaaaallah aaa
takabali yangu dua aaa aaallah
nakushukuru jalali,kwa huku kunizindua
ningepata idhwilaali,ningeiyaga dunia
nakushukuru jalali,kwa huku kunizindua
ningepata idhwilaali,ningeiyaga dunia
mimi ningekuwa wapi aaaaallah aaa
mauti yangenijia aaa aaallah
ningekimbilia wapi aaaaallah aaa
na wala hakuna njia aaa aaallah
illahi yule shetwani, asije nikaribia
umuweke mbali nami,hadi mwisho wa dunia
illahi yule shetwani,asije nikaribia
umuweke mbali nami,hadi mwisho wa dunia
ewe bwana mkarimu aaaaallah aaa
mwenye kukirimu waja aaa aaallah
sisi sote isilamu aaaaallah aaa
pepo yako twaingoja aaa aaallah
unipe kitabu changu,kwa mkono wa kulia
nakuomba mola wangu,mimi ninakulilia
unipe kitabu changu,kwa mkono wa kulia
nakuomba mola wangu,mimi ninakulilia
.....