Niguse Lyrics
- Genre:Spirituals
- Year of Release:2023
Lyrics
Niguse - Lgc Flavours
...
Nimeshagundua neno lako litahubiriwa
Kwa vyovyote vile utalifanya kuhubiriwa
Hata ukinituma nikatae litafikishwa
Utatumia chochote mwishowe litafikishwa
Yaani hata samaki, analisafirisha
Kushangaza hata punda, analiongea
Yaani hata kahaba, analifanikisha
Unatumia ndege kama njiwa kulifanikisha
.........
Hata nisiposifu,
Mawe yatakusifu
Nisiposema we bwana
Watoto watakiri
Hata nisiposifu,
Mawe yatakusifu
Ndio maana naomba uje uniguse mwenyezi
Mungu niguse,
Uwepo wako usiniishe
Moyo nikoshe,
Dhambi zangu nisafishe
Tena nitume,
Neno lako nifikishe
Kisha nivishe
Taji lako niringishe
........................
Yaani hata samaki, analisafirisha
Kushangaza hata punda, analiongea
Yaani hata kahaba, analifanikisha
Unatumia ndege kama njiwa kulifanikisha
.........
Hata nisiposifu,
Mawe yatakusifu
Nisiposema we bwana
Watoto watakiri
Hata nisiposifu,
Mawe yatakusifu
Ndio maana naomba uje uniguse mwenyezi
Mungu niguse,
Uwepo wako usiniishe
Moyo nikoshe,
Dhambi zangu nisafishe
Tena nitume,
Neno lako nifikishe
Kisha nivishe
Taji lako niringishe
.....................
Naomba nisamehe
Mwenyezi nirejeshe
Neno nifundishe
Kisha nitumie.