Pita Huku Lyrics
- Genre:Singeli
- Year of Release:2022
Lyrics
Pita Huku - Dulla Makabila
...
We mama mtu mzimaa ndoa ingekupa heshima
Kila kutwa mitandaoni ulidate na vitoto
Unadai mumeo anakitambi hawezi kupeleka moto
Awe mama pita huku
Uliaminiwa na kanisa
Ukaongoza kila misa
Ila ulijiona mungu mtu kisa unapesa sana
Uliamini ushirikina na kula kondoo wa bwana
Mchungaji pita huku
Kutwa unitukane ujachokozwa unagombana
Yani unalewa mpka unajikojolea
Ila swala la sadaka ulikua unajitolea
We mlevi pita huku
Najua umekata tamaa
Ndo mana nakuona umeshika tama
Najua umekata tamaa
Ndo mana nakuona umeshika tama
Yani kazi yako udj hilo halipingiki
Ila kila ulipofika muda wa ibada ulizima mziki
We dj pita huku
We kwanza unalaana chumbani kwako kuna mafuta kila kona
Unapenda kwa mparange mtume hataki ata kukuona
Ah we shoga pita huku
Nikikutazama unatia huruma
Mana naona utoboi
Ushawatoa mimba mina na zena
Na ulivyofundi hukosei
Nawe docta pita huku
Yani kufumba kufumbua ukajiona umefika
Sheria ukaipindisha
Masikini ukawakomesha
Na ukanenepa kwa rushwa
We hakimu pita huku
Wewe mtoto wakike ila nawe unadem
Na mademu wanakuita shemu
Aah inauma sana ata baba na mama hawataki ata kukuona
Maisha yako yote laana
Hauna mashine ila kazi tu kusagana
Tom boy pita huku
Malaya unafanya mtu anatelekeza mpaka familia
Ada ya watoto wake ikifika kwako unakoga bia
Yani kudanga bongo ulidhiki unaenda uturuku
Unakuvywa vidonge ata mimba ushiki
Mbele ya shemeji zako unapita na khanga
Malaya ukiamua lako unampa mpaka mganga
We malaya pita huku
Mchawi unafanya watu wanafukuzwa kazi
Wengine unawauwa kwakuwapa maradhi
Mchawi unawaachanisha mpka wapenzi
Mchawi unawanyima watu usingizi
Mchawi ooh nakosa chakuongea
Usiku unageuka paka mabati unarukia
Mchawi unauwa mtu anaacha familia
Msibani unatokea unalia hadi unazimia
Mchawi ndo chanzo cha umasikini
Unapita kwenye pembe hvi milango huioni
Na uchawi mkaupeleka usafini
Yani lavalava atembee vipi haonekani
We mchawi pita huku