Dunia Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Dunia - Hassan Mapenzi
...
Kuna kuvaa na kusitiri mwili
Kuna kuishi na kuishiaa wee!
Kuna kula na kujaza utumboo!
YOTE NI DUNIA oooo!
Unaogopa kuzama kwenye mapenzi
Unazama baharini unakufa
Unaogopa kuchepuka unabaki njia kuu
Lori linapita unakufaaaah
Unaogopa kushikwashikwa na mimi
Ukishikwa na korona unakufa
Unaogopa kusema yanayo kusibubuu
Unayaficha moyoni unakufaa
Dunia mwanangu
Tulia ila iyo yo yo
Dunia wewe
Tulia ila iyo yo yo
Oooh dunia
Mama alinifunza utuuzima ni ugwana
Mtaka cha uvunguni sharti kuinama
Mtaka vya kilele sharti kusimama
Leo me najioneaaah oooh
Unaempenda hajakupenda wewe
Anaekupenda hujampenda wewe
Mapenzi kichaka hayana hajenda
Waaminifu wengi wamekwendaaa
Dunia mwanangu
Tulia ila iyo yo yo
Dunia oooh
Ooh dunia
Mwanangu hutaki kazi
Kutegemea madanga
Ukipata maradhi unakufaa
Kaka unaleta mzaa weee
Kwenye mchezo wa ngumi
Unapigwa mchomoko inakufaaah
Dunia weeeeeoooh