Boomplay kusherehekea wasanii wa Afrika waliochaguliwa kwenye Tuzo za Grammy kwa kutoa Free Subscrip
Sekta ya muziki duniani inajitayarisha kwaajili ya usiku mkubwa wa mwaka kupitia tuzo za 65 zaGrammy. Huku wasanii wa Kiafrika wakipokea teuzi za kihistoria katika kategoritofauti mwaka huu.
App inayokua kwa kasi katika utoaji huduma yakupakua na kusikiliza muziki barani Afrika, Boomplay, imetangazakampeni ya kusherehekea tukio hili.
Boomplay inawapa watumiaji wake subscriptionya bure kufurahia na kugundua muziki bila vizuizi vyovyote na bila gharama kwasiku nzima, Jumatatu ya tarehe 6 Februari 2023, pale atakapotangazwa msaniiyeyote wa Kiafrika kushinda katika kategori zao.
Afrika inajivunia teuzi nane katika hafla ya mwaka huu, na angalau msaniimmoja wa Kiafrika akitarajiwa kurudi nyumbani na tuzo hiyo ya Grammy, hivyokuwafanya watumiaji wa Boomplay katika bara zima kusheherekea ushindi huokupitia App hiyo.
Tosin Sorinola,Mkurugenzi wa Idara ya Wasanii na Mahusiano ya Umma Boomplay, amesema: ''Boomplay imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono muziki na wasanii wa Kiafrika,na mpango wa subscription ya bure ni uthibitisho mwingine wa dhamira yetu yakuendelea kuwezesha mfumo wa muziki wa Kiafrika. Tunatoa subscription ya burekwa watumiaji wetu wote kwa ajili ya kusherehekea ubora wa muziki wa Kiafrikakatika tuzo za Grammy za 2023. Kupitia subscription hii ya siku moja bilamalipo, wapenzi wa muziki wanaweza kufurahia orodha yetu ya nyimbo zaidi ya milioni 95 ili kusikiliza maudhui bila matangazo na kupakua na kusikiliza bilabando, hii ni fursa nzuri kwa wapenzi wa muziki kuunga mkono na kusherehekeawasanii wanaowapenda. Tunajivunia kwa hatua kubwa zinazofanywa na wasanii wetuwa Kiafrika, kuuweka muziki wa Kiafrika kwenye ramani kimataifa, na hii ndiyonjia yetu ya kuwafurahia na kuwaunga mkono.''
Muziki wa Kiafrika uliwakilishwa vyema wakati Recording Academy ilipotoa orodha yake ya waliochaguliwa katikatuzo za 65 za Grammy. Mwimbaji nyota wa Nigeria Burna Boy na nguli wa BeninAngelique Kidjo wameteuliwa katika kipengele cha Albamu Bora ya Muziki yaUlimwenguni, huku Rocky Dawuni wa Ghana, Eddy Kenzo wa Uganda, Wouter Kellermanwa Afrika Kusini, Zakes Bantwini na Nombeco Zikode na Burna Boy wote wakiwaniakipengele cha Best Global Performance.
Cha ajabu ni kwamba, nje ya kategoria za Global Music, Tems wa Nigeria ameteuliwa katika kipengele cha Utendaji Bora waKuimba kwa Melodic na Wimbo Bora wa Rap kwa ushirikiano wake na Drake na Futurekwenye wimbo unaoongoza kwenye chati mbalimbali wa "Wait for You". Angelique Kidjo pia ameteuliwa katika kipengele cha Wimbo Bora uliowekwa kwenyekipengele cha Visual Media kwa Wimbo wake wa Woman King, "KeepRising".
Ikijulikana kwa vipengele vyake vilivyo rahisi kutumia na usikiliziaji wamuziki wenye sauti ya hadhi ya juu, Boomplay hutoa maktaba pana ya nyimbo napodikasti, pamoja na playlists zilizoratibiwa maalum kutoka kwa aina na wasaniimbalimbali, zinazosasishwa mara kwa mara ili kuhakikisha vibao vipya zaidivinapatikana.
Watumiaji wa Boomplay wanaweza kuunda orodha za kucheza, kugunduamuziki mpya kupitia mapendekezo maalum, na kusikiliza nyimbo nje ya mtandao.Mfumo wa usikilizaji hutoa uchezaji wa nyimbo zilizopakuliwa bila matangazo nanje ya mtandao kupitia subscription ya bei nafuu kwa siku, wiki na mwezi navifurushi vya bando kufuatia ushirikiano wake wa kimkakati na kampunizinazohusiana za mawasiliano.
Comments (17)
New Comments(17)
159047468
#Dogo D lujiga
iko bomba sana [0x1f608][0x1f621][0x1f621]
Kevini Sechele
هينتيزتيوةي
المعظم سدل طهنيدع ب[0x1f638][0x1f638][0x1f638][0x1f638][0x1f638]
هينتيزتيوةي
ممممسءرحيدراءظن ت ستاتاا [0x1f653][0x1f653][0x1f653]
Sankine Nzowadwubi
never give up
154820374
diamond platnumz
Ssanboy
diamond platinumz
space_tz
burna boy
Talki awadhi
Buln boy
Golden Junior_tz
Nice things
wewekuma