#BoomplayAwards: Alikiba abeba tuzo mbili kutoka Boomplay
Wanamuita 'Mfalme'. Staa wa muziki nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Alikiba amefanikiwa kushinda tuzo mbili 'Boomplay Plaques' kutoka Boomplay.
Alikiba ameshinda tuzo hizo mbili, ambapo tuzo moja ameipata kupitia wimbo wake wa 'Dodo' ambao umepata zaidi ya streams milioni 1 na tuzo nyingine ni ile inayohusu streams za jumla, ambapo amepata jumla ya streams milioni 10 kupitia ngoma zake zote zilizopo Boomplay.
Alikiba ni moja ya wasanii wachache na wa muda mrefu ambao wameendelea kuwa kwenye ubora ule ule na pengine unaoongezeka kila siku zinavyodizi kusonga mbele.
Tuzo hizi ni mwanzo mzuri kwa Alikiba hasa ikizingatiwa kuwa mwaka jana hakuwa amepata tuzo yoyote.
Mwaka huu ni dhahiri umeonekana ni 'kazi kazi' kwa staa huyu anayemiliki lebo ya Kings Music Records kutokana na kuachia ngoma kali 'back to back', ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.
Tayari amefanya ngoma tatu tangu mwaka huu uanze ambazo ni 'Ndombolo' ambayo wamefanya kama lebo ya Kings Music, 'Salute' ambayo amemshirikisha Rudeboy pamoja na 'Jelous' ambayo amemshirikisha Mayorkun.
Tayari ngoma hizo zimepata namba kubwa ya streams kwenye app ya Boomplay. Ndombolo imepata streams milioni 1.8, 'Salute' streams 1.8, na Jelous imepata streams 785.7k.
Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao wameahidi kutoa albamu mwaka huu, huku akisisitiza albamu hiyo itakuwa ngoma kali kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho.
Kwa sasa, Alikiba anatamba na wimbo wa 'Jelous' ambao unaendelea kufanya vizuri kupitia majukwaa mbalimbali nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.
Unadhani Alikiba atapata tuzo ngapi mwakani?
#BoomplayAwards #Alikiba #Music
Comments (116)
New Comments(116)
Felista Magoyo
Sharifad9htu
l love you Alikiba and song
Sharifu Mikongo
king Kiba umetisha sana
125446783
wenye kazi wapo kazin
Daudi Kasema
ggkihara1
king kiba twakutambua
125392589
I love you Alikiba❤️❤️❤️nice job congratulation
ciaraelezq
hongera
we love you Alikiba